Habari Mpendwa Bwana Yesu asifiwe.

Tuzungumze WEMA KATIKA UJANA. Kitabu ambacho nimekiandika hususani kwaajili ya vijana. Unajua kama Mungu anakupenda , kisha akamtoa mwana wake wa pekee Yesu kristo.sihitaji kukumbusha maana umesikia mara kadhaa. lakini ni upendo wa namna gani huu ambapo hata mzazi hawezi kuptia fedhea ya namna ile na maumivu yake ni makali.

Ila siku ya  leo napenda tuliongelee katika jicho la kusudi au mpango wa maisha .

Ndio, Yesu alikuwa na kusudi la kuja duniani na alilikamilisha , hakuangalia vipingamizi kama vita vya maneno, vita katika ufahamu, vipingamizi vya kisheria na mengineo. Bwana wetu alifuatilia mpango ili mimi na wewe tupate uzima wa milele . leo hii vizazi na vizazi vinanufaika na kukumbuka sadaka hii.

Yeremia  29:11

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.

Kijana mwenzangu nje ya mawazo au mpango wa Mungu hakuna amani wala tumaini mbeleni. tazama tumaini lililo ndani Yesu. tunamuhitaji Mungu kwa kutengeneza mahusiano nae kupitia Roho mtakatifu. Barikiwa  sana.

Ujajua kama mpango wa Mungu katika maisha yako ni Zaidi ya ufikiriavyo?

Changia mawazo kwenye coment hapo chini.