Bwana Yesu asifiwe mpendwa

Kijana wa karne hii ya kidigital unatakiwa kufahamu umuhimu wa watu katika maisha yako,Rasilimali watu. ndio maana Mungu alisisitiza kwenye upendo hata kwa adui yate ni kwa manufaa yako. Upendo unanguvu na ndio nguvu ya mahusiano baina ya mtu na mtu.

Watu ni mtaji ndio . Hakuna anaefanya biashara mwenyewe ,  wewe ni muuzaji unahitaji mnunuzi. Kijana wa kikristo, mpenzi wa Mungu, napenda kukumbusha katika safari ya kutukomboa, Yesu alihitaji watu ambao walikuwa wanafunzi.  

Kila unaemuona alipewa nafasi na watu kufika pale alipo. Mungu anatumia watu kukubariki. Yesu akiwa msalabani alikwenda mtu kuchukua mwili wake na kuupeleka kaburini, lakini hawa watu wawezi kukufikia kirahisi

Tufanye nini sasa ?

  • Tengeneza na Mungu kwanza . Mungu akiwa upande wako hakuna atakae kua kinyume na wewe warumi 8:31 . Yeye ndie awekekaye watawala . tengeneza mahusiano mazuri na Mungu. 
  • Kuwa mnyenyekevu. Wanyenyekevu ndio wanao rithi nchi mathayo 5:5
  • Thamini kazi na juhudi za waliokuzidi.Meza kiburi chako na uthamini kazi za mwenzio na kumshukuru Mungu kwaajili yao

Weka juhudi katika kila ufanyalo, iwe ni masomo , kazi, kipaji chochote. ukipata nafasi itumie vizuri na uhusishe ubora. Muulize Daniel .nakuambia tena watu wanaona hata pale ambapo unahisi upo pekeako. Taarifa zako zinapaa kwasababu ya watu wanaokuzunguka walio na ukaribu na watu wengine

Waombeee , njia nzuri ya kutengeneza mahusiano ya ndanikabisa na watu iwe wanakupenda au laa ni maombi. Kwa maombi yako Roho mtakatifu atawashuhudi. haina haja ya kujielezea sana au kushinda au kuonesha ubora wako kwa namna yeyote. maelezo hapo yanatosha kuvutia watu wenye mchango chanya kwenye maisha yako. Ubarikiwe