2 Wakorintho 10:3-6
3 Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani kama watu wa ulimwengu. 4 Silaha zetu si za kidunia, bali silaha zetu zina nguvu ya kimungu iwezayo kubomoa ngome.5 Tunaharibu hoja na mabishano yaliyo kinyume cha kumjua Mungu. Tunateka mawazo yote na kuyafanya yamtii Kristo,
Ukiona vitu vilivyo nje ya uwezo wako vinakusumbua na unashindwa kujinasua tambua uwepo wa nguvu nyuma yake
Na katika hili dhahiri ni nguvu za giza
Soma andiko hapo juu
Kunapo giza nuru lazima ingaze
Cha kwanza kabisa
Omba rehema... Ita damu ya Yesu ikutakase.. dhamilia ndani ya moyo ukimwamini Mungu.
Omba ujazo wa ROHO MTAKATIFU. Maana yeye ndie mtendaji mkuu. Tambua uwepo wake.
Ukimaliza hayo yote rudi kwenye ufahamu wako
Endapo yale mawazo yakikujia yakatae kwa kukiri kwa kinywa
Ukitaja Jina la YESU.
Rudia mpaka ufahamu wako ukae katika kumtii Kristo. Usijali yatapotea ukiwa muaminifu katika kukataa
Yakobo 1:14-15
Kabla ya tamaa kukupeleka kwenye kifo. Unatakiwa ukatae kwa kutamka
Barikiwa
0 Comments